TUMBI YASHINDA TUZO KWA UTOAJI HUDUMA BORA ZA MATIBABU

Posted on: September 15th, 2023

Hospitali ya Tumbi yashinda tuzo kwa utoaji huduma bora za matibabu. kupitia ukaguzi uliofanywa na Wizara ya Afya (Clinical Auditing) ambao umeiweka hospitali ya rufaa ya mkoa wa Pwani Tumbi kwenye nafasi ya mshindi wa tatu katika utoaji wa huduma bora za matibabu kati ya hospitali za rufaa za mikoa hapa nchini.