DAMU SALAMA
Posted on: December 21st, 2024KITENGO CHA DAMU SALAMA
Kitengo cha Damu salama hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani-Tumbi kilianzishwa rasmi mwaka……………..Kitengo hiki kipo chini ya maabara kuu ya hospitali ya mkoa wa Pwani-Tumbi na kinashughulikia maswala ya utoaji wa huduma ya damu salama kwa wahitaji wa damu ndani na nje ya hospital kwa kushirikiana na damu salama makao makuu kwa kufuata (Standards Operating Procedures -SOP) kwa ajili ya kuhakikisha mgonjwa anapata damu iliyo salama.
Hospitali ya Tumbi ina uhitaji mkubwa sana wa damu kutokana na wahanga wa ajali ukizingatia hospitali yetu ipo kando kando ya barabara kuu ya morogoro pia uhitaji upo kwa wagonjwa wengine toka sehemu mbalimbali . Kwa sasa kituo kinakusanya chupa 12-18 kwa siku , 60kwa wiki , 240 kwa mwezi wastani wa chupa 13 kwa siku sawa na chupa 65 waq wiki sawa na chupa 260 kwa mwezi. Kwa kiasi hiki kinakidhi mahitaji ila tunatakiwa kuongeza nguvu zaidi ili tuwe na akiba ya damu ya kutosha. Wadau wakuu wa uchangiaji damu ni wanafuzi, taasisi za dini,,majeshi na ndugu wa mgonjwa.
SHUGHULI ZA KITENGO
- Kusimamia na kuhakikisha usalama wa damu kwa wagonjwa
- Upatikanaji endelevu wa damu salama hospitalini
- Uchangiaji wa wa damu wa kila siku ndani ya kitengo.(walk-in donors)
- Utafutaji wa maeneo salama ya uchangiaji damu-( mashuleni, Vyuoni, makambini ,na kwenye jamii.)
- Upokeaji na Urudishaji wa majibu kwa waliochangia damu.
- Kutoa elimu sahihi kuhusu uchangiaji wa damu na kuhimiza umuhimu wa kupima afya kupitia kuchangia damu
- Unasihi wa ndugu wa mgonjwa na wachangiaji damu salama
Kitengo cha damu salama kinahitaji ushirikishwaji wa wadau mbalimbali wa kuchangia kwa hali na mali ili kupunguzia serikali mzigo