Huduma za Wagonjwa wa Nje

Posted on: April 24th, 2024

IDARA YA WAGONJWA WA NJE (OPD), DHARURA NA AJALI

Idara hii ni moja kati ya Idara zilizokamilika na kujitosheleza kihuduma. Katika mwaka huu 2022, Hospitali yetu ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani – Tumbi, kitengo cha majeruhi (Casualty) kilifanyiwa marekebisho makubwa yaliyopelekea kuzaliwa kwa vitengo viwili vya idara hii ambavyo ni Kitengo cha wagonjwa wa nje (OPD) na Kitengo cha wagonjwa wa dharura (EMD)

Katika idara ya wagonjwa wa nje tunahudumia wastani wa wateja 380 kwa siku. Tuna watumishi katika idara hii ikiwemo madaktari na wauguzi wanotoa huduma bora zinastohili kila siku. Ifuatayo ni orodha ya huduma zinazotolewa katika idara yetu ya wagonjwa wa nje.

WAGONJWA WA NJE (OPD)

  • Tunatoa huduma kila siku za kiafya kwa wahanga wa ukatili wa kijinsia kama vile kubakwa
  • Tunatoa huduma za uchunguzi wa afya kwa makundi mbalimbali kama wanafunzi na watu wengine wanaohitaji huduma kama hii kila siku.
  • Tunatoa huduma ya USHAURI NASAHA na upimaji wa VIRUSI VYA UKIMWI (VVU) bure kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa
  • Huduma ya kuonwa na daktari
  • Uchunguzi wa kitabibu
  • Huduma za vipimo kushirikiana na vitengo vingine kama vile maabara
  • Huduma za Elimu ya afya na Ushauri


KITENGO CHA WAGONJWA WA DHARURA (EMD)

  • Kuona wagonjwa wote wa dharura na kuwaimarisha kabla ya kwenda wodini au chumba cha upasuaji, au wodi ya wagonjwa mahututi.
  • Kufanya huduma za uchunguzi za dharura (P.O.C tests) kama vile (ECG, ABG, POC echo, FAST etc
  • Kutoa huduma ya dharura kuokoa maisha ya wagonjwa (lifesaving interventions)
  • Mafunzo ya utoaji huduma za dharura (Basic emergency care) kwa wafanyakazi wa idara, wafanyakazi kutoka hospitali zingine, wanafunzi wa ndani na nje ya nchi
  • Huduma za dawa kwa wagonjwa wa dharura
  • Tunatoa huduma ndogondogo za upasuaji kama vile kushona majeraha, kusafisha vidonda, na kuhudumia waliovunjika kila siku.