Upasuaji
Idara ya Upasuaji
Idara ya upasuaji ina vitanda 35 ambapo wodi ya wanawake upasuaji wa jumla na mifupa ni vitanda 14 na wodi ya wanaume upasuaji wa jumla na mifupa ni vitanda 21. Idara ya upasuaji wa jumla na wa mifupa vinapatikana katika jengo moja. Pamoja na chumba cha upasuaji (main theatre) na idara ya usingizi. Kwa upasuaji wa jumla siku za kliniki ni Jumanne na ijumaa wagonjwa huonwa na madaktari bingwa wa upasuaji. Na siku za upasuaji ni Jumatatu, jumatano na ijumaa. Alhamis ni siku ambayo wagonjwa wa wodini huonwa kwa kina na madaktari bingwa. siku za kliniki ya mifupa kliniki ni Jumanne na Alhamis ambapo wagonjwa huonwa na madaktari bingwa wa mifupa , siku ya jumatatu wagonjwa wa mifupa waliolazwa huonwa kwa kina na madaktari bingwa. Idara ya Upasuaji ni miongoni mwa idara sita za kitabibu zinazotolewa katika Hospitali ya Mkoa wa Tanga. Idara hii inafanywa na vitengo vitano ambavyo vimegawanywa kulingana na maeneo ya ubobezi/utaalamu. Vitengo hivi ni Upasuaji, Mifupa, Meno, Chumba cha Upasuaji. Jukumu kuu la Idara ni kuhakikisha huduma sahihi za upasuaji na zilizo boreshwa zinatolewa kwa wagonjwa wote.
Pia kinatoa huduma kwa wagonjwa wa dharura zinazosababishwa na ajali zinazopelekea kuumia sehemu ya kifua au tumbo.
Miongoni mwa Huduma zisizo za dharura zinazotolewa ni Upasuaji wa Ngiri, magonjwa ya mfumo wa nyongo, matiti, nk.
Pia tunatoa Huduma za upasuaji wa dharura kwa magonjwa kama vile upasuaji wa tumbo kutokana na maambukizi (peritonitis), kuziba kwa mfumo wa chakula (Intestinal Obstruction) na kuondoa sehemu ya mguu kutokana na madhara ya Kisukari(Diabetic foot) au mishipa ya damu(Gangrene).
Baadhi ya upasuaji wa magonjwa ya Urolojia yanayofanyika ni pamoja na tezi dume, kurekebisha Kibofu cha mkojo kilichoumia, kuwekewa njia mbadala ya kukojolea (SPC) kutokana njia ya mkojo kuziba.
Kitengo cha Upasuaji wa mifupa
Kitengo hiki kinajihusisha na magonjwa ya mifupa. Magonjwa ya dharura na yasiyo dharura ya mifupa. Miongoni mwa magonjwa yanayohitaji upasuaji wa dharura ni pamoja na Mivunjiko na mfupa nje ya kidonda (Open fracture), Kupoteza kiungo cha mwili katika ajali (Traumatic Amputation) pamoja na mteguko wa kiungo (dislocation).
Baadhi ya huduma za upasuaji kwa magonjwa yasiyo ya dharura yanayotolewa na kitengo hiki ni kama vile Jipu la mfupa, mivunjiko ya mfupa ya aina mbalimbali, mivunjiko ya mifupa isiyounga au kuunga vibaya, magonjwa ya viungo ya kuzaliwa nk.