Board

Bodi

Bodi ya ushauri ya hospitali ya mkoa wa Pwani_Tumbi ilizinduliwa tarehe Bodi ilizinduliwa tarehe 13/07/2020 na Muheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Bodi hii itakuwa hai kwa kipindi cha miaka mitatu tangu ilipozinduliwa.  bodi hii ina jumla ya wajumbe 13 wenye sifa tofauti na taaluma jumuishi ili kuleta uwiano wa kazi na ufanisi kiutendaji. 

  • ORODHA YA WAJUMBE WA BODI  YA USHAURI YA HOSPITALI HADI MWAKA  HUU 2022.

NA

JINA

WADHIFA

1

JASSON K. SHUMBUSHO

MWENYEKITI

2

DR. AMAANI MALIMA

KATIBU

3

DR. MARIAM ONGARA

MJUMBE

4

PHILEMON MSEGU

MJUMBE

5

ZILPA MREMI

MJUMBE

6

SALIM KAYANDA

MJUMBE

7

BENNO KIKUDO

MJUMBE

8

MAULID ABDALLA

MJUMBE

9

GUNINI KAMBA

MJUMBE

10

HERI H. MKUNDA

MJUMBE

11

MWITA IBRAHIM ISACK

MJUMBE

12

MTASHA A. SWEDI

MJUMBE

13

FILBERT BAYI

MJUMBE


MAJUKUMU YA BODI YA USHAURI 

Bodi ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwongozo huu wa “Uendeshaji wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa” unatambua uwepo wa “Mwongozo wa Uundaji, Usimamizi na Utekelezaji wa Majukumu na Kazi za Bodi ya Ushauri ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa (June 2016)”. 

Hivyo kama ilivyo kwenye mwongozo huo wa Uundaji,” majukumu ya Bodi ya (Ushauri) Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ni kama ifuavyo:

 a) Kushauri na kuidhinisha mpango mkakati wa Hospitali (Hospital Strategic Plan) na mpango wa uendeshaji wa Hospitali; 

b) Kusimamia, kufuatilia na kutathmini utekelezaji wa mipango kwa mujibu wa Sera na Miongozo ya Serikali; 

c) Kupitia na kuidhinisha Mpango wa Hospitali wa manunuzi kabla ya kuwasilishwa kwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya;

 d) Kusimamia rasilimali za Hospitali kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu zilizopo; 

e) Kusimamia, kushauri na kuimarisha uhusiano bora wa kiutendaji kati ya Hospitali za Rufaa za Mikoa, Uongozi wa Mkoa, na vituo vya kutolea huduma za afya ngazi ya Serikali za Mitaa;

f) Kushiriki katika kutafuta misaada, rasilimali mbalimbali na kupokea zawadi zinazotolewa na wadau Hospitalini; 

g) Kupitia na kushauri Wizara na Menejimenti ya Hospitali kuhusu makubaliano ya mikataba mbalimbali ambayo Hospitali inaingia na wadau mbalimbali; h) Kufanya vikao vya kawaida kila robo mwaka (Bodi inatakiwa kukaa vikao mara nne kwa mwaka); 

i) Kufanya vikao vya dharura inapobidi; 

j) Kusimamia ubora wa huduma zinatolewa katika Hospitali na kuhakikisha zinakidhi matakwa ya wananchi; 

k) Kuanzisha na kupitisha kamati ndogo ndogo zitakazotumika kutekeleza majukumu ya Bodi; 

l) Kupitia taarifa mbali mbali: kitaalam, utawala, manunuzi, fedha n.k. za robo mwaka na mwaka na kuziidhinisha; 

m) Kushughulikia maswala ya nidhamu za watumishi na malalamiko ya wateja na kumshauri Katibu Mkuu Wizara ya Afya juu ya hatua stahiki za kuchukua;

 n) Kubuni vyanzo mbalimbali vya mapato; 11

 o) Kuwasilisha Taarifa ya Utendaji na Taarifa ya Fedha kwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya kila robo mwaka kupitia kwa Katibu wa Bodi;