Obstetric and Gynacology
IDARA YA MAGONJWA YA MAMA NA MTOTO
Idara ya magonjwa ya mama na mtoto imegawanyika katika vitengo vitatu ambavyo ni wodi ya wazazi, wodi ya magonjwa ya wanawake na chumba cha upasuaji cha “Mama na Mtoto”.
HUDUMA ZITOLEWAZO
Tunajivunia kuwa sehemu ya hospitali za rufaa zinazotoa huduma bora kwa kina mama na kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi. Hii imefanikiwa kutokana na maboresho ya huduma na upatikanaji wa dawa na vifaa tiba kwa wakati.