Utawala
2.1. Uongozi na Utawala
Utoaji wa huduma bora utategemea misingi ya uongozi na utawala inayozingatia sheria, taratibu na
kanuni. Misingi hiyo itajumuisha uwajibikaji, usawa, uwazi na ushirikishwaji wa wadau wote katika
utoaji wa huduma za afya ikiwemo uwepo wa Bodi ya Hospitali inayowajibika ipasavyo.
Ili kuhakikisha utekelezaji wake unafanyika kwa uwazi: -
Menejimenti ya Hospitali inatakiwa: kufanya vikao kama ilivyoelekezwa kwenye miongozo
iliyotolewa na wizara; kutoa tarifa kwa mamlaka husika; kupokea maoni/malalamiko ya wateja
na watoa huduma na kuyafanyia kazi;
Kila Hospitali inatakiwa kuwa na utaratibu wa kutoa mrejesho kwa wadau wote kuhusu hatua
zilizofikiwa juu ya kushughulikia changamoto za uendeshaji wa Hospitali na utoaji wa huduma
za afya.
2.2. Rasilimali Watu katika Hospitali za Rufaa za Mikoa
Rasilimali watu katika Hospitali za Rufaa za Mikoa ni mojawapo ya nyenzo muhimu katika kutoa
huduma bora za afya. Serikali imefanya jitihada katika kuboresha rasilimali hii kwa njia mbalimbali,
ikiwa ni pamoja na kuongeza idadi ya wataalamu, kuboresha ujuzi katika nyanja mbalimbali, kuongeza
mishahara na maslahi mengine kwa watumishi. Pamoja na jitihada hizi, kuna changamoto kadhaa
zitokanazo na rasilimali watu zinazoathiri utoaji wa huduma za afya: -
upungufu wa watumishi/wataalamu katika hospital za Rufaa za mikoa,
uwiano wa ujuzi, usiokidhi (idadi ya wataalamu dhidi ya idadi ya watu) kulingana na ikama.
Sanjari na changamoto hizi, Wizara itaendelea kuwapanga watumishi waliopo kwa uwiano sahihi
katika Hospitali zote 28 za Rufaa za Mikoa. Aidha, usimamizi wa watumishi unatakiwa kuzingatia
sheria, taratibu na kanuni za utumishi wa umma zilizoidhinishwa na mamlaka husika. Hivyo: -
Timu ya Menejimenti ya Hospitali inatakiwa kushiriki kikamilifu kwenye uandaaji wa makisio ya
bajeti za mishahara ya watumishi kulingana na mwongozo wa Ikama na kuwasilisha kwa Katibu
Mkuu kila mwaka wa fedha;
Uongozi wa Hospitali unatakiwa kuhahikisha unasimamia watumishi waliopo kwenye maeneo
yao husika ili kuwezesha utoaji wa huduma bora kwa viwango vinavyokubalika;
Kusimamia utoaji maslahi na haki mbalimbali za kiutumishi;