BMG WATOA MSAADA KWA WAGONJWA TUMBI
Posted on: October 8th, 2025
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tumbi leo tarehe 11.10.2025 imepokea msaada kutoka BMG ambayo ni Kampuni ya Muziki kutoka Uingereza yenye Matawi 22 Dunia nzima ikiwemo Tanzania imerejesha tabasamu kwa wagonjwa wenye mahitaji mbalimbali kama viti vya wagonjwa ( wheelchair), Pampers, sabuni na mahitaji mengine muhimu kwa wagonjwa wenye uhitaji.
Aidha Mganga Mfawidhi wa Hospitali, Dkt. Amaani Malima, aliishukuru Kampuni hio kwa moyo wa upendo na kujali jamii, akisisitiza kuwa msaada huo utasaidia kuboresha huduma na kuwafariji wenye uhitaji.