KOFIH WAENDESHA MAFUNZO KWA WATOA HUDUMA ZA AFYA TUMBI

Posted on: August 27th, 2025

Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani Tumbi leo tarehe 28.08.2025 imepokea wageni kutoka Taasisi ya Korea Foundation for International Healthcare (KOFIH) ambao walikabidhi Vifaa Tiba na pia kuendesha mafunzo mafupi kwa watumishi wa idara ya dharura.
Miongoni mwa wageni waliotembelea hospitali walikuwa ni Prof. Kang Hyun, Lee ambaye ni Mtaalamu wa Dharura kutoka Yonsei University, Bi. Yoo Mi, Jeong ambaye ni Mtafiti na Mratibu wa miradi ya KOFIH, pamoja na Bw. Chan Young, Kang, EMT- Paramedic na Mtafiti kutoka Yonsei University pia waliambatana na Mwakilishi kutoka KOFIH Tanzania Bi. Josephine Kingi.

Mafunzo hayo yalilenga kuboresha uwezo wa watumishi wa dharura, katika kujenga ufanisi ufahamu wa changamoto mbalimbali na namna ya kuzitatua.

Aidha Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali Dkt. Erica Mrema alitoa shukrani kwa Taasisi KOFIH kwa mchango wao kwa kusema, Tunathamini msaada huu ambao utaboresha huduma za dharura na kuokoa maisha ya wananchi wengi. Ushirikiano huu ni ishara ya udugu wa kweli kati ya Tanzania na Korea Kusini ambao umekua endelevu kwa muda sasa.