MAADHIMISHO YA MIAKA 58 YAZINDULIWA KWA MICHEZO

Posted on: October 10th, 2025

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Dkt. Kusirye Okio ameyasema michezo ni furaha alipokuwa anafanya uzunduzi wa Tumbi Day leo tarehe 1 Oktoba, 2025 katika mchezo wa mpira wa miguu uliochezwa katika timu ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Tumbi na majirani zao Shirika la Elimu Kibaha.
Akiongea katika uzinduzi huo wa Maadhimisho ya miaka 58 toka kuanzishwa kwa Hospitali ya Tumbi, Dkt Kusirye Ukio ameupongeza Uongozi wa Hospitali kwa kuweka utaratibu mzuri wa kuwa na timu za michezo mbalimbali inayofanyika baada ya saa za kazi kwa ajili ya kupata furaha na faraja baada ya kazi ngumu ya kuhudumia wananchi wenye changamoto mbalimbali za kiafya.
Katika Maadhimisho hayo ya Tumbi Day yaliyozinduliwa leo yatashirikisha timu kutoka Taasisi za Umma mbalimbali kwa muda wa siku nne kuanzia leo tarehe 1 Octoba mpaka tarehe 4 Oktoba, 2025. Mechi hizi zote zitachezwa kuanzia saa 10.00 jioni kwa siku hizo zote.
Maadhimisho haya pia yataenda sambamba na utoaji wa huduma za afya bure kwa wananchi watakaofika katika kambi ya kutolea huduma itakayofanyika katika viwanja vya Mwendapole kuanzia tarehe 7 Oktoba, 2025 na kilele cha Maadhimisho haya kitakuwa tarehe 11Oktoba, 2025.
Mchezo wa mpira wa Miguu uliochezwa leo Timu ya Tumbi RRh imetoka na ushindi wa Goli moja bila bao ambalo limefungwa na Meshaki Kambona katika kipindi cha kwanza cha Mchezo.