MAFUNZO YA UFUATILIAJI NA TATHMINI (MONITORING AND EVALUATION) TUMBI
Posted on: October 23rd, 2025Watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani Tumbi, wamepata mafunzo ya Ufuatiliaji na Tathmini (Monitoring and Evaluation) yaliyoanza tarehe 20 Oktoba 2025 mpaka leo tarehe 24 Oktoba 2025, kwa lengo la kuwajengea uwezo kwenye kutekeleza majukumu yao ya kazi za kila siku.
Mafunzo haya yameandaliwa na uongozi wa hospitali kwa kushirikiana na wawezeshaji kutoka Wizara ya Afya ambao ni Ndg. Kiiza Kilwanila, Bi. Mwahija Hamisi, na Ndg. Andrea Ibrahimu.


