MTI WA UKUMBUSHO KWA HUDUMA ALIYOPATA TUMBI

Posted on: August 15th, 2025

Leo tarehe 15.08.2025 Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani Tumbi imeshuhudia jambo la kipekee na la kugusa mioyo, Bwana Ephraim Semu Massawe (Shamba Darasa) ambaye ni kati ya wagonjwa wanaopitia safari ya matibabu ya dialysis, leo hii amepanda Mti ( American Palm) katika hospitali yetu. Mti huu si wa kawaida bali ni alama ya matumaini, ishara ya uzima, na somo kwamba hata katika nyakati ngumu, mtu anaweza kuacha alama chanya kwa vizazi vijavyo alisema Bwana Massawe.
Aidha Kaimu Mganga Mfawidhi Dkt. Pius Muzzazi aliongezea kwa kumshukuru Bwana Massawe kwa moyo wake wa upendo na kumuombea afya njema, nguvu na maisha yenye baraka. "Mungu aendelee kumlinda na kumwongezea siku nyingi za furaha".