MWEZI WA UELIMISHAJI KUHUSU UGONJWA WA SIKOSELI

Posted on: September 18th, 2025

Leo tarehe 18.09.2025 katika Kuadhimisha Mwezi wa uelimishaji kuhusu ugonjwa wa SIKO SELI, ( SEPTEMBER AWARENESS MONTH) Dkt. Pius Muzzazzi, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya watoto, aliongoza kikao cha kitaalamu cha wahudumu wa afya katika Kituo cha Afya cha Mkoani, Kibaha Pwani.

Katika mawasilisho yake, Dkt. Muzzazzi alizungumzia kuhusu nafasi ya watoa huduma za afya katika matibabu, njia za kuzuia na athari za ugonjwa wa SIKO SELI katika jamii, . Pia alibainisha kuwa Tanzania inashika nafasi ya tatu barani Afrika na nne duniani kwa idadi ya wenye SIKO SELI, hali inayohitaji juhudi za pamoja katika kutoa elimu na huduma bora ili kukata mnyororo wa ugonjwa huu.

Aidha, Dkt. Muzzazzi aliwahimiza wananchi kupima ili kubaini kama ni wabebaji wa vinasaba vya SIKO SELI (sickle cell carriers) au la. Alisisitiza umuhimu wa kupima kwa ajili ya kulinda vizazi vijavyo dhidi ya kuendelea kuathirika na ugonjwa huo.

Kikao hiki kililenga kuongeza uelewa kwa watoa huduma za afya, kubadilishana uzoefu, na kuimarisha mikakati ya kutoa msaada endelevu kwa wagonjwa SIKO SELI nchini.