STANBIC YATOA MSAADA HOSPITALI YA RUFAA YA RUFAA YA MKOA WA PWANI - TUMBI

Posted on: October 9th, 2025


• Ni sehemu ya mpango endelevu wa kusaidia jamii kwa kuchangia uboreshaji wa sekta ya Afya.

Benki ya Stanbic imetoa msaada wa vifaa tiba vyenye thamani ya Shilingi Milioni 60,000,000 kwa Hospitali ya Mkoa wa Pwani ikiwa ni sehemu ya ushiriki wa Benki hiyo katika maendeleo ya jamii kwani ina wajibu wa kuhakikisha jamii inayowazunguka inafaidika kutokana na faida wanayoipata.

Akizungumza leo Ijmaa Oktoba 10, 2025 wakati wa hafla ya makabidhiano ya vifaa tiba hivyo, Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wandani Ndugu Omari Nkiga amesema Benki ya STANBIC ni kinara katika kujali na kujihusisha na masuala mbalimbali ya jamii hapa nchini na kwamba changamoto za sekta ya afya Tanzania kwa benki ya STANIC ni jambo la kipaumbele, na hii ni kutokana na ukweli kwamba afya ni mtaji wa maendeleo kwa taifa lolote hapa duniani.

Katika makabidhiano hayo yaliyoshuhudiwa na Mganga Mkuu wa Mkoa Pwani Dkt. Kusirye Ukio, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani, Dkt. Amaani K. Malima na Menejimenti ya Hospitali Benki hiyo wamekabidhi vifaa mbalimbali kama vile viti vya Magurudumu (Wheel chairs), Magodoro, Vifaa Tiba na vifaa vya kufanyia Usafi vyote kwa pamoja vinathamani ya shilingi Millioni 60.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Pwani Dkt. Kusirye Ukio ameishukuru benki hiyo kwa kuwapa msaada huo na kisha kueleza kwamba sekta ya afya inapitia changamoto nyingi na amewapongeza sana kwa wao kuliona hilo na kuja kutoa msaada huo