TAASISI YA KOFIH YATEMBELEA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA PWANI-TUMBI
Posted on: June 25th, 2025
TAASISI YA KOFIH YATEMBELEA HOSPITALI YA TUMBI.
Leo tarehe 24 Juni, 2025 timu ya watu saba kutoka taasisi ya Korea Foundation for International Healthcare (KOFIH) wametembelea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani – Tumbi. Lengo la maafisa hawa likiwa ni kufuatilia miradi iliyofadhiliwa na taasisi hyo na kuangalia shughuli mbalimbali za Hospitali zinavyoendeshwa. KOFIH iliwezesha hospitali ya Tumbi kupatiwa mashine na vifaatiba mbalimbali ambavyo vimekuwa msaada mkubwa katika utoaji wa huduma mbalimbali za afya.
Akitoa shukrani kwa Maafisa hao wa KOFIH Dkt. Amaan Malima, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Pwani – Tumbi ameishukuru Taasisi ya KOFIH pamoja na Serikali ya Korea kwa misaada ya vifaatiba mbalimbali waliyoitoa kwa Hospitali kwa kusema vifaatiba hivyo vimesaidia sana katika kutoa huduma mbalimbali za afya kwa wananchi. Akitaja maeneo ambayo Taasisi hiyo walifadhili ni eneo la afya katika huduma za wajawazito na uzazi, watoto wachanga, mashine ya kutakasa vifaatiba, ununuzi wa jenereta la kisasa, ununuzi wa mashine ya ufuaji nguo pamoja na upanuzi wa jengo la watoto waliochini ya uangalizi maalum.
Maafisa waliokuwa kwenye msafara huo ni Bwn. Changi Ho Lee (CEO,GCK Co., Ltd Director, Global Together), Prof. Sunjoo Kang, Gyeongbae Seo (Mwakilishi wa KOFIH Tanzania), Bwn. Joonhyoung An ( Vice President, STN sports TV/News), Dkt.Yoo Rha Hong (Neonatologist, Associate Professor, Department of Pediatrics, Kosin University College of Medicine), Prof. Jee Young Lee (Assistant Professor, Department of Microbiology, Kosin University College of Medicine) na Bi. Josephine Kingi (Msimamizi wa Ofisi KOFIH Tanzania.
Katika ziara yao hospitalini Tumbi timu hivyo iliongozana na maofisa wa ngazi mbalimbali wa wa hospitali na watembezwa kwenye maeneo mbalimbali kati yay ale waliyo toa msaada wa vifaatiba kama vile wadi za wazazzi na upasuaji , watoto wachanga, sehemu ya genereta la kisasa, wadi ya watoto wachanga, sehemu ya kufulia nguo na jengo la watoto waliochini ya uangalizi maalum.