TUMBI YAADHIMISHA SIKU YA WAFAMASIA
Posted on: September 25th, 2025
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani -Tumbi Leo tarehe 26.09.2025 imeadhimisha Siku ya Wafamasia Duniani kwa matukio maalumu yaliyopangwa na Idara hii husika. Kwa Kufungua tukio hili rasmi Mganga Mkuu Mfawidhi Dkt. Amaani Malima aliwashukuru watumishi wa idara ya famasi kwa mchango wao muhimu katika kuboresha huduma za afya, nakusisitiza kuwa juhudi zao ni nguzo kubwa katika kuwahudumia wagonjwa na kuimarisha ustawi wa Hospitali na jamii kwa ujumla.
Kwanza, kulikua na zoezi la kuchangia damu kama ishara ya kuokoa maisha. Pia, watumishi hao walikata keki kama alama ya mshikamano na kutambua mchango wa wafamasia katika huduma za afya. Mwisho, wafamasia walitembelea wodi ya watoto (paediatric ward) na kuwashika mkono watoto kama ishara ya upendo, tabasamu na faraja.
Kauli mbiu ya mwaka huu inasema: “Fikiria Afya, Fikiria Mfamasia” ikitukumbusha umuhimu wa wafamasia katika kuimarisha huduma za afya na maisha pamoja na jamii.