Kliniki ya Methadoni

Posted on: March 4th, 2024

kliniki ya methadoni ni moja ya kliniki zinazofanyakazi siku saba kwa wiki (Kila siku) matibabu ya emthadone hutolewa kwa waraibu wa dawa za kulevya ambao wameamua kuachana na madawa ya kulevya na kujiunga na mpango wa matibabu maarufu kama MAT. katika kliniki hii huduma mbalimbali hutolewa ikiwemo utolewaji wa dawa ya methadoni, matibabu ya mabadiliko ya kitabia na huduma za ziada kwa wateja wenye matatizo ya kiafya kama waathirika wa ugonjwa wa Ukimwi, Kifua kikuu na Homa ya Ini. vile vile huduma za upimaji wa afya na msaada wa kinasihi hutolewa, pia huduma za chanjo ya Uviko 19.