Kliniki ya Huduma na Kinga (CTC)

Posted on: December 13th, 2024

KLINIKI YA HUDUMA NA KINGA (CTC)

Kituo cha ushauri nasaha na kupima cha hospitali ya rufaa ya mkoa wa pwani kilianza kazi rasmi tarehe 15  Juni,2005.Kituo kilianza na chumba kimoja kikiwa na jumla ya  wateja wapatao 10.Mwaka mmoja baadae kulifanyika juhudi kukapatikana vyumba 6 ,vyumba viwili kwa ajili ya madaktari,chumba kimoja kwa ajili ya ushauri nasaha,chumba kingine kwa ajili ya kutolea dawa,chumba kwa ajili ya masijala na kingine chumba cha takwimu za wateja .Msaada huu ulitolewa na shirika lisilo la kiserikali la EAGPAF ambao ndio walikuwa wafadhili wa kituo chetu kwa wakati huo.

Mnamo mwaka  2010 kulikuwa na ongezeko kubwa la wateja ilipelekea shirika lisilo la  kiserikali linalofadhiliwa na watu wa marekani la ICAP ambao ndio walikuwa wafadhili wa kituo chetu wakati huo kutoa msaaga wa kutujengea jengo jipya kwa ajili ya  CTC lenye vyumba 14 ,kati ya vyumba hivyo ,vyumba vitatu ni kwa ajili ya madaktari,vyumba viwili kwa ajili majijala na takwimu za kituo,vyumba viwili kwa ajili ya famasi,chumba kimoja kwa ajili ya maabara ndogo,kimoja kwa ajili ya kufanyia vipimo vya virusi vya ukimwi,chumba kimoja cha manesi,chumba kimoja kwa ajili ya kuweka appointment za wagonjwa,chumba kimoja kwa ajili ya afisa lishe na afisa ustawi wa jamii,chumba kimoja kwa ajili ya washauri rika na kimoja kwa ajili ya kutolea huduma ya uzazi wa mpango.

Hadi Kufikia Septemba 2019 kituo kilikuwa kimeandikisha jumla ya wateja 11,135, kati ya hao 3,515 wanaume na 7,620 wanawake.Pia kituo kimeweza kuwaanzishia wateja 6,999 dawa za kupunguza makali ya virusi vya ukimwi ,kati ya hao walioanzishiwa wanaume 2,290 na wanawake 4,709

Huduma zitolewazo kituoni ni pamoja na:

  • Huduma rafiki kwa vijana wanaoishi na maambukizi ya VVU
  • Ushauri wa ufuasi sahihi wa dawa
  • Ushauri nasaha kwa wapokea huduma wenye wingi mkubwa wa VVU
  • Uchunguzi na ushauri wa lishe
  • Ushauri wa kisaikolojia (Social counseling )
  • Uzazi wa mpango
  • Minor laboratory for minor investigation ie.HB Level,BS-mps,RBG and sample collection viral load,CD4,LTF,RTFand FBP
  • Uchuguzi wa saratani ya shingo ya kizazi
  • Ushauri nasaha na upimaji wa virusi vya ukimwi.


 

WASIFU WA KLINIKI YA AFYA YA UZAZI YA BABA,MAMA NA MTOTO

Kliniki ya afya ya uzazi ya baba,mama na mtoto inatoa  huduma zifuatazo:Upimaji wa mimba,Huduma ya mama na mtoto baada ya kujifungua,huduma za chanjo kwa watoto baada ya kuzaliwa,upimaji wa VVU kwa baba na mama,upimaji wa saratani ya shingo ya kizazi,huduma za kuzuia maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto(PMTCT) ,huduma za daktari bingwa wa magonjwa ya kinamama.

Huduma za kuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa motto zilianza rasmi mwezi Aprili mwaka 2007 kikiwa na jumla ya wapokea huduma 23,kati yao 15 wakiwa wajawazito ,3 kinamama wanao nyonyesha, 5 kina baba na watoto 4.

Mpaka kufikia September 2019 kulikuwa na kina mama wajawazito 1312 walio andikishwa. Kliniki ya afya ya uzazi ya baba,mama na motto inapatikana katika hospitali ya tumbi

 

KLINIKI INATOA HUDUMA ZIFUATAZO:

  • Ushauri na upimaji wa VVU kwa kina mama wajawazito na wenzi wao
  • Kuwatambua watoto mapema kama wameambukizwa VVU
  • Kuwapa matibabu wakina mama wajawazito na wanao nyonyesha wenye maambukizi ya VVU na dawa ya kinga kwa watoto waliozaliwa na kina mama wenye VVU.
  • Ushauri wa kisaikolojia
  • Huduma ya uzazi wa mpango
  • Uchunguzi na ushauri wa lishe
  • Uchuguzi wa saratani ya shingo ya kizazi kwa watu wanaoishi na VVU
  • Utoaji wa dawa za kufubaza VVU (ARVs)na dawa kwa ajili ya magonjwa nyemelezi
  •  Huduma za chanjo