Internal medicines
Idara ya magonjwa ya ndani
Idara ya magonjwa ya ndani ndiyo idara yenye historia ndefu Zaidi katika hospitali yetu kutokana na tatizo lililopelekea kufunguliwa kwa Hospitali yetu kua miongoni mwa magonjwa yanayohudumiwa na idara hii. Idara ya magonjwa ya ndani ipo katika sakafu ya mwanzo katika jingo la Galanos na imegawanyika katika sehemu kuu 3, wodi ya A1, A2 na Magonjwa ya akili. Idara hii ipo Wodi ya A1 na A2 zimetengwa kwaajili ya wanaume na wanawake huku wodi ya magonjwa akili ikiwa eneo upande wa kushoto wa geti la kuingilia. Idara hii hutoa huduma mathubuti kwa wagonjwa wote wenye magonjwa ya ndani na yanayohitaji utaalamu/ubobezi kama vile magonjwa ya moyo, kisukari, Akili nk. Huduma hizi za kitabibu hutolewa na jopo la madaktari wa ngazi tofauti wakiongozwa na madaktari wabobezi katika idara ya magonjwa ya ndani. Kiasi cha wagonjwa 500 hupatiwa huduma kila wiki
Idara ya magonjwa ya ndani kwa kushirikiana na Chuo cha Afya na sayansi shirikishi Tanga (TIHAS) hutoa mazingira mazuri kwaajili ya mafunzo kwa wanafunzi wa utabibu pamoja na madaktari walioko katika mafunzo ya utarajali.